Nyimbo za Kristo 194
Twaomba Baraka Zako
Tune: Nyimbo za Kristo 24
1Twaomba,
Bwana‿umpokee Kama mhudumu;
Ambaye‿anajitoa Kuwa mtumishi.
2Twaomba,
Bwana‿umpokee Kama mhudumu;
Neno lako‿alitoe,
Mwangaza kung'aa.
3Mwokozi wetu, twaomba, na‿umwandikie
Kitabuni mwako juu
Mjumbe wa injili.
4Silaha zake‿apewe Kumshinda adui;
Vitani awe hohari,
Mpaka mauti.
5Yeye ashindaye, Bwana,
Kwa rehema yako,
Ile taji ya dhahabu,
Nawe utampa