Nyimbo za Kristo 20
Mungu Wetu Yeye Mwamba
1Mungu wetu yeye mwamba,
Kimbilio taabuni;
Msaada penye shida ulio karibu sana.
RefrainMwamba wetu kutupumzisha, yu kivuli kuburudisha,
Yu Mwongozi katika njia, kimbilio taabuni,
2Mchana usiku, yule kimbilio taabuni,
Hivyo hatutaogopa, kwani yu karibu sana.
3Iwayo yote,
Yeye tu kimbilio taabuni,
Twamjua Yeye Mlinzi aliye karibu sana.
4Mungu wetu Ficho kwetu, kimbilio taabuni,
Siku zote uwe Boma lililo karibu sana.