Skip to content

Nyimbo za Kristo 21

Baba Twakujia

Tune: Church Hymnal 599

1Baba twakujia,
Uwe msaada;
Uwe kimbilio, twakusihi.
Dunia ni giza tukitengwa nawe;
Tufariji hapa, Baba yetu.

RefrainBaba twakujia, tu dhaifu, usitugeue, tusikie.

2Salama tulinde, kati ya taabu;
Uwe raha yetu mashakani.
Roho yasumbuka, Baba tujalie;
Twakuomba sana, tupe nguvu.

3Neema utupe, tukubali kwako;
Moyo wetu Linda, safarini;
Tuongoe mbele, tupate kushinda
Na kufika ng'ambo, kule kwako.