Nyimbo za Kristo 3
Mungu Atukuzwe
1Mungu atukuzwe kwa mambo makuu,
Upendo wake ulitupa Yesu,
Aliyejitoa maisha yake,
Tuwe nao uzima wa milele.
RefrainMsifu, msifu, dunia sikia;
Msifu, msifu, watu wafurahi;
Na uje kwa Baba, kwa Yesu Mwana,
Ukamtukuze kwa mambo yote.
2Wokovu kamili, zawadi kwetu,
Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu;
Wanaomwamini na kuungama,
Mara moja wale husamehewa.
3Alitufundisha mambo makuu,
Alihakikisha wokovu wetu,
Lakini zaidi, ajabu kubwa,
Yesu atakuja na tutamwona.