Nyimbo za Kristo 33
Karibu Sana
Nearer, Still Nearer
Tune: Church Hymnal 390
1Karibu sana univute, karibu sana daima niwe.
Bwana napenda unishike,
Unilinde nisitengwe nawe,
Unilinde nisitengwe nawe.
2Karibu sana, sina kitu,
Sina sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu:
Uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.
3Karibu sana wewe nami,
Ninafurahi kuacha dhambi‿Anasa zote na kiburi:
Nipe Yesu niliyemsulibi,
Nipe Yesu niliyemsulibi.
4Karibu sana, hata mwisho.
Hata mbinguni nisimamapo:
Daima dawamu niwepo
Nitakapoona uso wako,
Nitakapoona uso wako.