Nyimbo za Kristo 57
Usikatae Kazi
Tune: Christ in Song 513
1Usiikatae kazi yake Bwana;
Ukae tayari kuifanya kazi;
Uende po pote Mungu akwitapo,
Nawe utaona furaha kazini
RefrainNjoo,
We!
Usikatae;
Njoo,
We!
Uifanye kazi;
Usiikatae kazi yake Bwana,
Ili hatimaye usikatazwe juu.
2Usiikatae kazi yake Bwana;
Kwa nini kawia?
Fanya kazi leo.
Mavuno meupe,
Wachache wavuni,
Onyesha furaha Kwa kazi ya Bwana.
3Usiikatae kazi yake Bwana;
Kukataa pendo Kwako ni hatari.
Saa ya rehema, Yesu akiomba,
Ziungame dhambi,
Zifutwe mbinguni.