Nyimbo za Kristo 64
Piga Panda Ya Injili
1Piga panda ya Injili, onyesha watu wote;
Ili anayesikia atubu, aokoke.
RefrainPiga panda ya Injili, upige kwa nguvu;
Mungu amekuagiza mateka wawe huru.
2Upige vilimani, kwa kila tambarare;
Pande zote, miji yote isikie Injili.
3Uipige mipakani, barabarani pia;
Iwatangazie wote, wanakwitwa na Baba.
4Uipige!
Watu wengi wataka wawe huru;
Waambie kwamba Yesu asema Njoni kwangu.