Skip to content

Nyimbo za Kristo 63

Niuonapo Msalaba

When I Survey the Wondrous Cross

Tune: Church Hymnal 120

1Niuonapo msalaba,
Kristo‿aliponifia;
Kwangu pato ni hasara.
Kiburi nakichukia.

2Na nisijivune, Bwana,
Ila kwa sadaka yako;
Upuzi sitaki tena,
Zi chini ya damu yako.

3Tangu kichwa hata nyayo,
Zamwagwa pendo na hamu,
Ndako pweke hamu hiyo.
Pendo zako zimetimu.

4Vitu vyote vya dunia,
Si sadaka ya kutosha;
Pendo zako zaniwia,
Nafsi, mali, na maisha.