Skip to content

Nyimbo za Kristo 65

Twendeni Askari

Studio

1Twendeni askari,
Watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele,
Tumwandame juu;
Ametangulia Bwana vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.

RefrainTwendeni Askari,
Watu wa Mungu;
Yesu yuko mbele,
Tumwandame juu.

2Jeshi la shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia;
Kelele za shangwe zivume pote;
Ndugu, inueni zenu sauti.

3Kweli kundi dogo, watu wa Mungu,
La mababa yetu ni letu fungu;
Hatutengwi nao, moja imani;
Tumaini moja, na moja dini.

4Haya mbele watu nasi njiani,
Inueni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa yake Mfalme;
Juu hata chini sana zivume.