Skip to content

Nyimbo za Kristo 69

Cha Kutumaini Sina

Studio

1Cha kutumaini sina ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha.

RefrainKwake Yesu nasimama,
Ndiye mwamba: ni salama;
Ndiye mwamba: ni salama.

2Njia yangu iwe ndefu yeye hunipa wokovu;
Mawimbi yakinipiga nguvu zake ndizo nanga.

3Damu yake na sadaka nategemea daima,
Yote chini yakiisha Mwokozi atanitosha.

4Nikiitwa hukumuni,
Rohoni nina amani;
Nikivikwa haki yake sina hofu mbele zake.