Nyimbo za Kristo 73
Bwana, Uniongoze Juu
1Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu;
Naomba nikisafiri,
Bwana uniongoze juu.
RefrainBwana uniinue juu Kwa imani hata mbingu.
Juu kuliko dunia;
Bwana uniongoze juu.
2Moyo wangu hautaki Kukaa palipo shaka;
Wengine wapenda chini Nia yangu ni kupanda.
3Nataka kupanda juu Nisishindwe na adui;
Kwa imani nasikia Sauti ya washindaji.
4Kupanda juu nataka Niuone utukufu;
Hata mwisho nitaomba,
Bwana uniongoze juu.