Skip to content

Nyimbo za Kristo 76

Mrithi Ufalme

Studio

1Mrithi ufalme, kwani walala?
Karibu wokovu wasinzia?
Amka, simama, uvae silaha,
Haraka sana, saa zapita.

2Mrithi ufalme mbona 'kawia?
Mbona hupokei zawadi?
Haya, uvae,
Mwokozi yuaja;
Haraka, umlaki afikapo.

3Mataifa makuu ya dunia!
Yapigana kujiangusha Usisihofu dalili, mrithi;
Ishara zote hazikawii.

4'Sitazame anasa za dunia,
Kwani hayo yapita upesi;
Zivunje kamba zinazokufunga;
Mrithi ufalme, njoo 'karudi.

5Inua kichwa, tazama mbele tu,
Mfalme aja na utukufu;
Jua laonekana milimani,
Warithi ufalme furahini.