Skip to content

Nyimbo za Kristo 74

Niambie, Ee Mlinzi

Watchman, Tell Us of the Night

Tune: Church Hymnal 180

1Niambie,
Ee mlinzi,
Umepambazuka je!
Utukufu wa Zayuni,
Pana dalili zake?
Msafiri‿uondoke,
Utazame mbinguni,
Kiunoni ujifunge,
Ni kucha alfajiri.

2Mlinzi‿inamulika Nuru njiani mwako,
Dalili za kuja kwake,
Kwamba siku karibu;
Panda itakapolia Itawaamsha wafu,
Watakatifu wa Mungu,
Kuwapa kutokufa.

3Mlinzi, ione nuru
Ya mwaka wa Sabato;
Sauti zinatangaza Ufalme ni karibu;
Msafiri ninaona Mlima wa
Zayuni,
Mji wa Yerusalemi
Nayo fahari yake.

4Kwenye mji wa dhahabu
Anaketi mfalme Katika kiti kizuri: huku anatawala.
Pana amani po pote,
Mashamba husitawi;
Na ardhi ina rutuba;
Mito ni mitulivu.

5Mlinzi, twaribia Nchi iliyo nzuri;
Twende mbele, tufurahi,
Nchi inachangamka,
Sikieni kuna wimbo
Wa waliookoka;
Kaza mwendo,
Ujiunge Na kundi
Kubwa hili.