Skip to content

Nyimbo za Kristo 75

Msini Imara, Ninyi Wa Bwana

How Firm a Foundation

Tune: Church Hymnal 255

1Msingi imara, ninyi wa Bwana,
Umewekwa kwenu kwa neno lake.
Nini zaidi atasema Bwana,
Imani yenu ipate kuzidi?
Imani yenu ipate kuzidi?

2Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka haitazidi;
'Takuwapo nawe, nikuwezeshe,
Shida upatazo zisikutishe!
Shida upatazo zisikutishe!

3Utakapopishwa ndani ya moto
Nguvu nitakupa, upate pato;
Huteketezwi, ila taka zako.
Nazitasalia dhahabu zako.
Nazitasalia dhahabu zako.

4Na mtu aliye nitegemea
Nguvu za Jehanamu zijapotisha,
Kamwe kwa adui sitamtia;
Mtu wangu kamwe sitamwacha.
Mtu wangu kamwe sitamwacha.