Skip to content

Nyimbo za Kristo 78

Mpaka Lini Bwana

Studio

1Mpaka lini Bwana,
Utakaa mbali?
Kumetuchosha moyo kukawia hivi.
Utatujia lini,
Ili tufurahi Katika ile nuru, kuja kutukufu?

2Mpaka lini Yesu,
Utaacha watu Uliowakomboa,
Wawe na mashaka?
Wachache waamini,
Kwamba utarudi;
Wachache wa tayari,
Bwana kukulaki.