Nyimbo za Kristo 79
Nataka Imani Hii
O for a Faith That Will Not Shrink
Tune: Church Hymnal 245
1Nataka Imani hii:
Imani imara,
Ambayo haitetemi Kitu chote
Wakati wa shida,
Wakati wa shida.
2Isiyonung'unika Huzuni, taabu;
Lakini katika saa ya matata
Humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.
3Imani inayong'aa katika tufani;
Isiyoogopa giza, wala shida,
Njaa na Hatari,
Njaa na hatari.
4Haiogopi dunia,
Kudharau kwake;
Haiangushwi na hila, na uwongo
Dhambi na ogofyo,
Dhambi na ogofyo.
5Bwana, nipe‿imani hii,
Hivi nitaweza Kuonja hapa chini ulimwenguni,
Kurithi furaha,
Kurithi furaha.