Skip to content

Nyimbo za Kristo 90

Mapya Ni Mapenzi

New Every Morning Is the Love

Tune: CS1908 794

1Mapya ni mapenzi hayo,
Asubuhi tuonayo;
Saa za giza hulindwa,
Kwa uzima kuamka.

2Kila siku, mapya pia,
Rehema, wema na afya,
Wokovu na msamaha,
Mawazo mema, furaha.

3Tukijitahidi leo Na mwendo utupasao,
Mungu atatueleza Yatakayompendeza.

4Mamboyetu ya dunia Bwana atayang'aria,
Matata atageuza Yawe kwetu ya baraka.

5Yaliyo madogo, haya Bwana tukimfanyia,
Yatosha: tutafaidi Huvuta kwake zaidi.

6Ewe Bwana, siku zote,
Tusaidie kwa yote:
Mwendo wetu wote vivyo,
Uwe kama tuombavyo.