Nyimbo za Kristo 91
Kaa Nami
1Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani,
Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu kaa nami.
2Siku zetu hazikawi kwisha;
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi;
Usiye na mwiso, kaa nami.
3Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani Ila wewe Bwana, kaa nami.
4Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako kaa nami.
5Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikiwe;
Nuru za mbinguni hazikomi;
Siku zangu zote kaa nami.