Nyimbo za Kristo 93
Jua La Rohoni Mwangu
1Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu;
Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.
2Nikipata usingizi, nijaze fikira hizi,
Nitamu sana, nilale pendoni mwako milele.
3Kaa nami, ewe Bwana, usiku kama mchana,
Nisiishi mbali nawe; ni uhai kuwa nawe.
4Kama mtoto mnyonge ameshawishwa atange,
Mtafute Ewe Bwana, ujirudishie tena.
5Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini,
Waliao,
Mtulizi, wape wote usingizi.
6Asubuhi tutokapo, tukaribie tulipo;
Twingiapo duniani tuwe mwako mkononi.