Skip to content

Nyimbo za Kristo 94

Po Pote Mashamba Yajaa

Studio

1Popote mashamba yajaa tele nafaka pevu,
Popote yang'aa meupe bondeni na nyandani.

RefrainMwenye mavuno twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.

2Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo wakusanye ko kote.

3Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake na furaha kuu.